Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawamke CUF (JUKE) ambaye pia alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu Kigoma Kaskazini, Kiza Mayeye amejiondoa rasmi leo kwenye chama cha CUF na kujiunga na ACT Wazalendo.
Mayeye amekitumikia Chama Cha Wananchi CUF kwa nafasi mbalimbali tangu mwaka 2011 alipojiunga, mwaka 2020 aligombea Ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini na kwa matokeo halisi alishinda. Mayeye amesema yeye ni mwanasiasa wa vitendo anaamini siasa halisi ipo chini kwa wananchi.
โNimejiunga ACT Wazalendo ili kuendeleza mapambano, nimefanya uchambuzi wa kina na kijiridhisha kuwa chama hiki ndio jahazi sahihi la kuendeleza harakati zangu kwa ajili ya kuwakomboa wananchi wa Kigoma Kaskaziniโ, amesema.
Aidha ameongeza kuwa amevutiwa na sera za ACT Wazalendo za kujenga Tanzania ya wote kwa maslahi ya wote kwa kushawishika na jitihada za chama kwa kuimarisha mtandao wake kwa nchi nzima na pia kwa chama kukuza vipaji vya vijana na wanawake.
About The Author
Last modified: May 30, 2023