Visit Sponsor

Written by 12:32 pm KITAIFA Views: 14

SERIKALI KUGHARAMIA MATIBABU KWA MAJERUHI NA MAZISHI YA WANAFUNZI WA AJALI – BAHI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Serikali itagharamia mazishi ya Wanafunzi wawili (2) wa shule ya sekondari  Mpalanga Wilayani Bahi waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea jana majira ya saa 5:00 asubuhi katika Kijiji cha Chidilo  Wilayani humo.

Aidha, Mhe. Senyamule ameahidi kuwa, Serikali itagharamia matibabu ya wanafunzi wote majeruhi31 walioumia katika ajali hiyo ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Ajali hiyo imehusisha gari yenye namba za usajili T 519 BSY aina ya Mitsubishi Canter mali ya Bw. Abdul Rashid mkazi wa Dar es Salaam. Gari hiyo ilikuwa imebeba wanafunzi 51, walimu wawili na dereva mmoja ambao walikuwa wakielekea Shule ya Sekondari Magaga kushiriki mashindano ya michezo ya UMISETA

Kwa mujibu wa Mkuu wa Usalama barabarani Wilaya ya Bahi, ASP Bakari Ramadhani amesema kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari hilo lililobeba wanafunzi, uliosababisha gari kumshinda dereva, kuacha njia na kupinduka na hadi sasa dereva wa gari hiyo anashikiliwa na jeshi la polisi.

Akitoa salamu za Serikali Mhe. Senyamule amewataka wafiwa kuwa na moyo wa subra na kuelekeza Jeshi la Polisi kuchukua hatua haraka kwa wote watakaothibitika kuhusika na uzembe kwa namna yoyote ile.

“Ndugu zangu nawapa pole kwa niaba ya Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.Tumeguswa sana na misiba hii ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa la leo na kesho. Serikali iko pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu, tutaendelea kushirikiana katika wakati huu wa msiba kwa kusimamia mazishi ya marehemu na matibabu ya majeruhi wetu. Viongozi wote wakuu pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa anaSerikali za Mitaa (TAMISEMI) mwenye dhamana ya kusimamia Shule na Michezo mashuleniwanatoa pole sana” Mhe. Senyamule.

About The Author

(Visited 14 times, 1 visits today)

Last modified: May 30, 2023

Close